Kununua magari kutoka Japani Kwa mnunuzi kwa mara ya kwanza

Hatua 11 Unazotakiwa Kuzifahamu ili Uweze Kuagiza Gari Zilizotumika Toka Nchini Japan

Last updated:

Tutakupatia dondoo muhimu na kuzielezea kiundani kuhusu jinsi ambavyo wanunuzi wapya wa magari wanaweza kununua magari yaliyotumika toka Japan kwa usalama kabisa.



1. Wakati wa kuchagua gari unalazimika kuchagua msafirishaji (exporter) pia

-Unapochagua gari, ni lazima kuchagua exporter (msafirishaji).

-Japokuwa kuna makampuni mengi yanayouza magari yaliyotumika mtandaoni, hapa tumekukusanyia yale ambayo ni maarufu Zaidi katika orodha ifuatayo.

-Japokuwa makampuni maarufu Zaidi yanaashiria uaminifu na usalama, hatuwezi kusema kwa uhakika kabisa yakuwa magari yao yana bei sahihi au yapo katika hali sahihi ya kuridhisha.

-Unachopaswa kuelewa ni kwamba, kampuni maarufu na hata zile ambazo sio maarufu pia huwa wananunua magari katika minada ileile. (wananunua magari sehemu moja).




2.Wasafirishaji (Exporters) Wote wa Magari Yaliyotumika Huyanunua Katika Minada

-Exporters wengi wa magari toka Japan huwa wanayanunua katika minada maalum inayofanyika nchini Japan.

-Minada hufanyika mtandaoni na katika maeneo zaidi ya 70 ndani ya Japan kila wiki. Washiriki wa minada hii huwa ni wengi sana na hata makampuni makubwa ya kuuza magari nje (yaliyoorodhesha hapo juu) hushiriki minada hii.

-Katika mnada mkubwa zaidi nchini Japan ambao hufanyika USS Tokyo, karibu magari 10,000-15,000 huuzwa kwa siku, na wazabuni wapya hujitokeza karibu kila baada ya sekunde 10.

-Kwa idadi hii ya magari yanayouzwa, magari mengi ya aina moja huzuiliwa. Ikiwa yana hali na muundo unaofanana, basi bei ya mwisho ya kuuzia mara nyingi hufanana pia. Na bei hizi ndizo tunaziita bei elekezi za manunuzi kulingana na wazabuni.

-Kwa Mfano, Rav 4 ya mwaka 2005 (ZCA26W) ikiwa katika hali nzuri kiasi na imetembea umbali wa kilomita 100,000 inaweza kuwa na bei inayolingana mnada mmoja hadi mwingine kulingana na bei elekezi za manunuzi kulingana na wazabuni.




Una Mashaka Kwanini Gari Fulani Iuzwe Bei ya Chini Sana?

Wasafirishaji na wauzaji magari wa nchini Japan hununua magari moja kwa moja kakika minada.

Kurahisisha Zaidi, ili kuweza kuwa mshindi na kuuziwa gari fulani katika minada hii ya magari, mzabuni lazima ataje, bei ya juu kuwadhihirishia wauzaji utayari wake wa kununua gari husika. Na kwa sababu hakuna mzabuni yeyote aliye tayari kununua gari kwa bei ya juu kuliko bei elekezi za minada, bei za kununulia magari hutokana na wazabuni walio tayari kununua gari kwa wakati huo, na wao ndio hupanga bei.

Unaweza kutafuta aina Fulani ya gari (aina ya gari, modeli yake, rangi, umbali iliotembea, mafuta n.k) kutoka kwa wauzaji tofautitofauti.

Hizi tovuti mara nyingi huwa na bei zinazofanana kwa magari yanayofanana vigezo, na hii ni kwa sababu makampuni hununua magari kwa kuzingatia bei elekezi za minadani.
 
Kutokana na kuwepo tofauti za bei minadani, kuna mazingira mauzo hufanyika kwa bei za chini sana. Tunashauri wakati wa kufanya manunuzi ufanye ulinganifu wa bei za wauzaji na bei elekezi za minada na serikali.


Sababu za kuwa na magari yanayouzwa chini ya bei elekez:

  1. Endapo gari limedumu sokoni kwa zaidi ya miezi mitatu (huwekwa kwenye kundi la kuuzwa kupunguza msongamano))
  2. Ikiwa gari lipo katika hali mbaya, linaweza kuuzwa kwa bei pungufu ya bei elekezi
  3. Ikiwa mteja wa kwanzan ataingia katika kashfa nahatopewa gari hilo hata kama amelilipia, basi gari hurui sokoni na kuuzwa kwa bei pungufu

Endapo gari itaingizwa katika kundi la magari yaliyokaa muda Mrefu na kuhitajika kuondoshwa kwenye yadi mara nyingi pia gari hizi huwa katika hali mbaya.
Kimsingi, ikiwa gari limepunguzwa bei tunapaswa kufikiri na kufahamu kwanini imekuwa hivyo.

Tutakwenda kujadili namna ya kujua bei elekezi ya soko kwa ajili ya gari unayoitaka na namna ya kukwepa kuingia katika kashfa au kufanya bisahara na wauzaji wadanganyifu.

Unapata kile unachokilipia, na huu huwa ni msemo maarufu sana maeneo mengi duniani Japan nayo ikiwemo, na bila wasiwasi kabisa huu ni ukweli usiopingika..




3.Fahamu Kuhusu Gharama za Kusafirisha Magari Yaliyotumika

Tovuti nyi za wasafirishaji wa magari nje ya Japan utazikuta na taarifa au maelezo yafuatayo:

Bei ya FOB Hii huitwa Base vehicle price
Mizigo na Uchukuzi Usafirishaji kuja nchini kwako.
Kulingana na bandari yakupokelea mzigo utakayoichagua, na ukubwa wa gari, bei hutegemea ukubwa wa gari lakini wakati mwingine bei huwa haibadiliki.
Bei za C&F (CFR) Hii inasimama badala ya maneno Cost (bei yagari) na freight (usafiri).
Hii ni jumla ya FOB pamoja na Freight vikiwekwa pamoja. Manunuzi kwa kutumia bei za C&F ni njia sahihi Zaidi inayojali thamani ya fedha yako katika usafiirishaji wa magari. Lakini bima ya usafiri wa majini huwa sio sehemu ya gharama hizi.
Bei ya CIF Hiki ni kifupisho cha maneno Cost (“bei ya gari”, bima (insurance) pamoja na usafirishaji (freight). Kimsingi hii ni sawa na C & F lakini imeonezewa bima ya usafirishaji baharini.
Bima ya kusafirisha mizigo baharini (Marine insurance) Fidia endapo upotevu/uharibifu wa gari utatokea (ikitokea ajali na meli ikazama kwa mfano). Bima hii mara nyingi itatoka tu endapo kumekuwa na upotevu wa gari na sio uharibifu.
Ukaguzi kabla ya gari kutumwa Ukaguzi unaweza kufanyika kabla ya gari kutumwa. Kabla ya gari kuondoka Japan, lazima likaguliwe, kwa upande wa wasfirishaji ukaguzi huu huuita JEVIC, JAAI, na QISJ.
Gharama za usafirishaji nchi kavu Hizi ni gharaka za kusafirisha gari toka bandarini hadi maeneo ya mbali na bandarini. Ushuru wa kuingiza magari nchini kwako sio sehemu ya gharama hizi.
Gharama za ziada Kila kampuni ya usafirishaji huwa na gharama zake.





Ni Vitu Gani Hujumuishwa Katika Gharama Unayomlipa Msafirishaji wa Gari Toka Japan Kuja Kwako?

Malipo yafuaayo hujumuishwa katika gharama unazowalipa wasafirishaji:

Ni pamoja na

  1. Gharama ya gari
  2. Gharama ya kulisafirisha toka bandarini mpaka kukufikia ulipo (ikiwa sio FOB)
  3. Bima ya kusafirishamagari/mizigo kwa kutumia bahari
  4. Gharama za ukaguzi wa gari kabla ya kulituma (hiari)
Hazijumuishi

  1. Ushuru wa forodha bandarini (nchini) kwako) inajumuishwa tu endapo itahusisha huduma za usafirishaji katika nchi zisizo na bandari)
  2. Ushuru wa kuingiza/kuagiza magari na kodi zingine za ndani
  3. Ada za usajili wa magari

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kuagiza gari kutoka nje, ada za jedwali la pili hapo juu zitakuwa na umuhimu kwako ndani ya muda mfupi ujao. Kwa Mfano, itakuwa tatizo kubwa sana endapo hutoweza kulipia ushuru bandarini kwako wakati gari lako litakopowasili bandarini.




5.Ni kwanini kampuni za uchukuzi wa mizigo na magari huwa na bei tofauti ikiwa umbali na mzigo ni uleule na hupelekwa kwenye bandari hiyohiyo?

Ukitizama magari yenye ukubwa unaolingana katika tovuti za wasafirishaji tofautitofauti na kulinganisha bima za usafiri baharini, gharama za usafirishaji, na gharama za ukaguzi, utagundua kuwa gharama ni tofauti.

Bila shaka, gharaa zao hutofautiana kulingana na huduma na ukubwa wa kampuni husika.
Hata hivyo, sababu ya msingi ya kutofautiana huku ni ni kwakuwa faida ya jumla itokanayo na usafirishaji wa magari hutofautiana kwa kila kampuni.

Mgawanyo wa bei za wasafirishaji (exporters)

Kwanza, tutizame gharama za kulitoa gari toka Japan hadi nchini mwako.

Gharama ya Gari Thamani ya gari lenyewe
Gharama za kuitoaa gari nje ya Japan Gharama za usafiri wa nchi kavu toka mnadani hadi bandarini, gharama za yadi, gharama za C&F wa Japan, nakadhalika.
Gharama za uchukuzi Gharama za uchukuzi kwa makampuni ya usafirishaji toka Japan hadi nchini mwako

Gharama za mauzo ni jumla ya gharama zole tajwa pamoja na faida ya wachukuzi.

Gharama (bei ya gari + ada ya kutuma nje ya japan + ada ya ucukuzi) + faida= Bei ya kuuzia gari


Bei za Magari kwa Wanunuzi wa Nje ya Japan

Bei za magari kwa wanunuzi wa nje ya Japan huwa na mwonekano huu

Bei ya FOB: Gharama ya gari + gharama za usafirishaji + faida
Mzigo: Gharama ya kusafirishia + faida

Pointi ya msingi ni hii, kwa makampuni ya usafirishaji baadhi hayahusishi faida na ada ya kusafirisha katika bei za FOB, badala yake huyaweka katika gharama za usafirishaji..
Kuna nyakati makampuni kwa makusudi kabisa hufanya bei za FOB kuonekana kuwa chini ilihali wanakuja kuongeza gharama za usafirishaji.

Kwa Mfano:

Bei ya FOB: bei ya gari - mabadiliko ya bei iliyotangazwa (*) (*)
Usafirishaji: gharama ya usafiri + mabadiliko ya bei iliyotangazwa (*bei hiyohiyo)



Ukitizama gharama za gari ambazo zina muundo na modeli sawa, tafadhali zingatia Mfano huu hapa chini.

Kwa Mfano:
Ikiwa gharama ya gari ni $1,200,
Gharama za usafirishaji ni $500,
Gharama za mzigo (gari) $1,000,
Na faida kwa wauzaji $300

Kampuni A Bei ya FOB : $2,000
(bei ya gari + uasfirishaji + profit)
Uchukuzi wa mzigo : $1,000
Kampuni B Bei ya FOB: $1,200 Uchukuzi wa mzigo: $1,800
(gharama za uchukuzi+ gharama za kuexport + faida)
Kampuni C Bei ya FOB: $1,000
(bei ya gari- mabadiliko ya bei iliyotangazwa mwanzo)
Uchukuzi wa mzigo: $2,000
(gharama za uchukuzi+ gharama za kuexport +faida+ mabadiliko ya bei iliyotangazwa)

Kama ambavyo umeona hata kama jumla ya gharama ikiwa inalingana kwa makampuni yote (dola $3,000 ktk mfano huu) bado Bei ya FOB inaweza kuonekana, kanakwamba ni nusu ya gharama. Kuwa makini na wasafirishaji hawa ambao wanajaribu kupata faida kwa mtindo huu.

Endapo utakuwa na maswali baada ya kuona kiasi hiki cha bei ya FOB, utagundua kuwa bei ya jumla ya gari husika haitofautiani sana ukiangalia jumla kuu.

Hakikisha unafanya ulinganifu wa gharama ya jumla ya kusafirisha gari, (kuna wakati unalazimika kujua gharama za ukaguzi wa kabla gari halijatumwa pia).




6.Namna ya Kuangalia Taratibu za Usafirishaji na Ushuru

Kuhakiki Ushuru wa Kusafirisha Magari

Ukilinganisha na bei za magari yanayouzwa eneo unapoishi, unaweza kuona kanakwamba bei za wauzaji wa magari ya Japan ziko chini sana.
Hii ni kwa sababu bei za kuuzia magari hazijumuishi gharama za ushuru wa kusafirisha magari.

Ushuru wa kuingiza magari unaofautiana nchi moja hadi nyingine. Na mara nyingi ushuru unaweza kufikia asilimia 100% ya bei ya CIF. Kwahivyo ili kuweza kuelewa ni kiasi gani gari itakugharimu, ni vyema ukaangalia ushuru wa kuingiza gari nchini mwako.

Hakikisha unatembelea mamlaka ya mapato ya nchini mwako kujua ushuru halali wa kuagiza na kuingiza gari nchini mwako.

Kuhakiki Taratibu Kuagiza Magari

Ni muhimu kutafuta na kujua taratibu za kuingiza gari nchini mwako. Taratibu za kuingiza magari kwenye nchi nyingi zinakuwa na taarifa kama hizi zifuatazo:

  1. Ni marufuku kuingiza gari za kuendeshea mkono kushoto/kulia
  2. Miaka inayoruhusiwa kwa gari kuwa limetumika kabla ya kuliingiza nchinimwako (Mf. Nchini Kenya lazima lisizidi miaka 7)
  3. Magari yaliyotumika hayaruhusiwi kuingizwa nchini. (Mfano China na Afrika kusini wamepiga marufuku kuingiza magari yaliyotumika toka Japan.)

Ikiwa utahakiki gari zilizotumika na kisha kugundua haziruhusiwi nchini mwako, itakuwa ni kazi bure kwahivyo ni vyema ukajua taratibu za kuingiza magari kutoka nje ya nchi yako.




7.Kuhakiki hali ya Gari

Kabla ya kufanya manunuzi, zitizame picha zilizopostiwa kwa umakini kuhakiki hali ya gari.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kuhakiki picha

Angalia ikiwa kuna baadhi ya maeneo ya gari yameharibika na hivyo kufutwa katika picha. Mf gari kuoneshwa upande mmoja tu ni kiashirio cha tatizo. Ikiwa kutakuwa na baadhi ya maeneo hayaoneshwi inapaswa kukufanya uwe na mashaka kwa mba inawezekana kuna tatizo mahali Fulani.

Tumewahi kusikia tukio moja ambapo mteja alinunua gari likiwa linaonesha picha za maeneo mengi isipokuwa mlango wa dereva. Mteja alikuja kugundua baadae kuwa, mlango wote ulikuwa umelika karibu ya kung’oka. Ikiwa una mashaka yoyote kwa upande wako ni vyma ukawasiliana na muuzaji.

Kuhusu injini, Kuna wakati picha zinaweza zisionekane vizuri kuonesha ikiwa Kuna tatizo.
Utalazimika kuwa makini zaidi endapo bei ya gari husika ipo chini zaidi ya bei elekezi ya soko la magari kwa wkt huo.

Kuna wakati inatokea, japo si mara nyingi sana, gari likaondoka Japan likiwa zima na matatizo yakajitokeza wakati wa usafirishaji baharini.

Japokuwa baadhi ya kampuni za usafirishaji hazina msaada linapotokea tatizo la aina hii, zipo kampuni baadhi ambazo hutoa fidia endapo kunakuwa na tatizo la aina hii katika usafirishaji wa gari lako.




8.Mambo ya kuzingatia wakati wa kutuma fedha ng'ambo

Kabla yakununua gari ulitakalo, hakikisha unafanya uhakiki wa bei ya modeli hiyo sokoni kwa wakati huo, ushuru wa kusafirisha gari, na taratibu zingine muhimu za nchini mwako.

Hizi zifuatazo ni taarifa muhimu zinazohitajika wakati wa kulipia gari mtandaoni:

  1. Utolewaji wa profoma invoice
  2. Usafirishaji wa nyaraka za mauziana
  3. Utumwaji wa slipu za benki (copy za TT)
  4. Uwasilishaji wa ada za kutolea fedha nchini Japan na hitimisho la mikataba

Ikiwa mmeafikiana vigezo vya kuuziana gari, oma kampuni itakayosafirisha gari lako ikupatie hati ya malipo.
Kabla ya kufanya manunuzi, hakiki taarifa zilizojazwa katika profoma invoice.

Tahadhari

Hakiki kwa umakini sana taarifa zinazohusiana na akanti za benki na taarifa zilizojazwa katika profoma invoice.

Majina ya Akaunti ni:

  1. Mara nyingi hili ni jina la kampuni linalomiliki tovuti yenye gari ulilochagua
  2. Ikiwa upo katika tovuti ya CardealPage auTradecarview, kampuni inayohusika hapo ni Cardealpage wenyewe au Tradecarview na sio vinginevyo

Hata hivyo, ikitokea jina la akunti likawa tofauti kabisa na taarifa zilizoandikwa katika profoma invoice, kuna uwezekano kukawa na ulaghai na hivyo unalazimika kuhakiki na muuzaji wa gari kabla hujalinunua na kulipia..

Ikiwa profoma invoice imekwisha tolewa, unaweza lutembelea benki ili kutuma fedha.

Uhamishaji wa fedha utakapokamilika, utapatiwa risiti na kopi ya TT kutoka benki na hivyo ni lazima kutuma kopi hiyo ya TT haraka kwenda kwa kampuni ya uuzaji magari.
Kwa wauza magari walio wengi, baada ya kuwa wamepokea kopi ya TT watalihifadhi gari kwa ajili yako na hatauziwa mtu mwengine tena.

Muda unaohitajika fedha kufika Japan

Muda unaotumika ili fedha kufika nchini Japan endapo malipo yamefanyika nchi nyingine yanategemeana na nchi husika. Mara nyingi siku kadhaa (siku 2-5) zinahitajika.

Ikitokea zimepita zaidi ya siku 5 na hujasikia chochote toka kwa muuzaji wa gari, wasiliana na benki yako.

Mara tu malipo yanapowasili nchini Japan, kampuni inayokuuzia gari itatoa notisi kuonesha kukamilika kwa mkataba baina yenu.




9.Gari haitaondoka Japan kwa haraka, inachukua muda kiasi

Muuzaji wa gari atanza mchakato wa kusafirisha gari yako mara baada ya kuwa wamepokea malipo. Weka akilini mwako kwamba, fedha kuwafikia haimaanishi kuwa wataanza mchakato muda na siku hiyohiyo.

Mpaka gari kupakiwa kwenye meli, inachukua angalau wiki 1. Mchakato wa kusafirisha gari toka Japan huwa na kuonekano huu hapa chini.

  1. Uhakiki wa hali ya gari (yapo makampuni mengi ambayo hayafanyi uhakiki)
  2. Kusafirisha gari kwenda katika eneo linapohakikiwa kabla ya kupakizwa melini
  3. Kupeleka gari katika yadi ya wakala wa kutoa na kusafirisha magari
  4. Kufanya matayarisho (booking) ya mahali pakuliweka gari melini
  5. Kufanya michakato ya lazima ya bandarini
  6. Kufanya ukaguzi wowote ule kama meli inayosafirisha magari ikihitaji ufanyike
  7. Kupakiwa gari katika sehemu maalum ndani ya meli

Bila kutegemea sehemu gari husika linapopelekwa, ni kawaida kwa nafasi lilipopakiwa gari melini kuwa na muda wa kati ya mwezi mmoja mpaka miezi mitatu.

Baada ya kukubaliwa kupewa nafasi ya kusafirishia gari ndani ya meli, hupaswi kuwa na hofu endapo hutapata mawasiliano yoyoyte toka kwa wenye meli kwani wao huwasiliana na wauzaji wa magari.

Ikitokea kwa bahati mbaya gari lako lisipakiwe melini mpaka ukapita mwezi mzima baaada ya kuwa umelipa, kunaweza kuwa na tatizo kwa hivyo wasiliana na aliyekuuzia gari.

10.Maandalizi ya Kutoa Gari Bandarini

Mara gari lako litakapowasili bandarini, ni lazima liatapitia hatua za kawaida za kutoa mizigo bandarini kwa mujibu wa taratibu za nchi yako.
Hakikisha unawasiliana na wakala (agent) wa clearing and forwarding ili kujadili nae ni kwa namna gani anaweza kukusaidi na malipo yake.

11.Baada ya Gari Kuondoka Bandarini

Mara baada ya meli kuondoka bandarini, ndani ya siku 4-5 kampuni inayoimiliki meli husika hutuma B/L yaani bili ya shehena kwenda kwa kampuni iliyokuuzia gari.
Baada ya hapo kampuni iliyokuuzia gari, itakutumi nyaraka hiyo kwa kutumia mawakala kama DHL au Fedex.
Uwasilishwaji wa nyaraka hii kwa mteja hufuata taratibu za nchi husika mteja alipoa.

*Makabidhiano ya nyaraka ni ya lazima ili kuhakiksha kwamba unalipokea gari lako baada ya kuwa limesafirishwa na kwa kawaida nyaraka zinaweza kushana na gari kwa muda wa siku kadhaa.


12.Mandalizi Bandarini kwako

Wiki moja kabla ya gari lako kuwasili, clearing ajenti wako lazima afanye maandalizi yanayotakiwa ili kurahisisha upoklewaji wa gari.

Nyaraka zotte za msingi zitakopukuwa zimepokelewa, ikiwa ni B/L au cheti toka kwa muuzaji wa gari, hakikisha unakabidhi nyaraka hizi haraka iwezekavyo kwa mtoa mizigo (clearing agent).

Mambo ya kuzingatia wakati wa kupokea gari

Unapopokea gari lako angalia kiwango cha oil. Ikiwa oil ni kidogo sana au imekwisha ijaze upya ndipo uwshe Injini ya gari.

Baada ya kuwa imewaka, iache iungurume tu hata kwa dakika 10 na baada ya hapo unaweza kuitembeza. Inapokuwa melini, mara nyingi oil hutolewa kama tahadhari dhidi ya moto melini kwahivyo endapo utaendesha gari pasipo kuweka oil nyingine Injini yako itaungua.


Mpaka sasa, tumezungumzia juu ya mambo ya msingi ya kuyaweka akilini unapoagiza gari toka Japan.

Unapoagiza gari toka Japan, unaweza ona yakuwa upo uwezekano wa kupata gari zuri kwa bei nafuu kabisa ikilinaganishwa na kununulia gari nchinikwako.

Tunashauri yakuwa ujaribu kujitathmini uwezo wako mwenyewe na kuona utakapoishia hata kama hujawahi kuagiza gari toka Japan.
 
Pata gari kutoka katika tovuti ya CardealPage sasa.
https://www.cardealpage.com/

-Kununua magari kutoka Japani, Kwa mnunuzi kwa mara ya kwanza

Copyright© CardealPage , 2024 All Rights Reserved.