Taarifa muhimu Uelewa

Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia Katika Kununua Lori za Mitsubishi (Mitsubish Canter). Sehemu ya 01

Last updated:

Katika tovuti ya CardealPage, Tunaweka picha nyingi sana za canter za Mitsubishi,  na  Canter Guts .

Bei ni kitu cha msingi sana, lakini pia ni muhimu kuelewa uwezo na sifa za gari husika ili kufanya maamuzi sahihi na kununua gari linaloendana na mahitaji yako.

Nitaelezea mambo 10 ya kuzingatia wakati wa kununua canter.


1. Kuchagua muundo wa sehemu ya abiria na dereva kwa matumizi tofautitofauti

Nchini Japan, malori yana matumizi tofautitofauti kama yalivyoainishwa hapa chini.

  • Malori yakubeba uchafu (takataka), mchanga, vifusi vya udongo, n.k.
  • Malori yenye bodi maalum za kubeba mizigo ya kawaida.
  • Malori maalum (power gates) kwa ajili ya kubeba mizigo mizito.
  • Lori zenye migongo mirefu (bodi ndefu) pamoja na bodi fupi za kubebea mizigo pamoja kazi zingine.
  • Canter maalumu (powergates) za kuinulia mizigo mizito na kuweka katika bodi au kupakua kutoka kwenye bodi kushusha chini.
  • Malori yenye bodi ngumu za aluminiamu kwa ajili ya kubeba mizigo pasipo kuonekana (kwa sababu ya kiusalama).
  • Lori za zenye fokolift na bodi maalumu kwa ajili ya kuinua na kubeba mizigo mizito. Mfano, mzigo wa vigae, idadi kubwa ya makaratasi, au vizuizi/matofali ya barabarani.
  • Lori zenye winchi maalum za kupakiza na kushusha mizigo mizito.

Swali la msingi, Unahitaji lori (canter) ya aina gani? Ngoja tukusaiie kupata aina ya lori litakalofaa na kuendana na biasharayako.

Canter/Lori zinazohifadhi baridi Canter (Lori) za vifusi/takataka Canter za kuinua vitu juu
Canter zenye bodi flati Canter zenye bodi ndefu Canter za power gate
canter normal canter power gate
Canter zenye bodi ngumu za aluminiam Canter zenye bodi za muundo wa mbawa Canter zenye winchi


2. Chagua kulingana na idadi ya abiria watakaopakia canter

Ni watu wangapi wanaweza kusafri na canter yako?

Kwa kawaida canter zinakuwa na mstari (row) mmoja, lakini zipo baadhi ya canter zinakuwa na mistari (rows) miwili ya kukaa na aina hii huitwa “double cabin”.

Double cabin huwa ni nzuri endapo umepanga lori lako libebe  Zaidi ya watu (abiria) wanne (4). 

Ikiwa ungependelea abiria wa ziada watumie sehemu ya nyuma ya canter kama kitanda, (kitu ambacho ni hatari haswa kwa safari ndefu au safari za mwendo kasi), basi double cabin ni chaguo sahihi kwa matumizi ya aina hii.

Ili kutafuta double cabin ndani ya tofuti (kurasa) ya CardealPage, chagua lori na kisha chuja (punguza) wingi wa matokeo kwa kutumia idadi ya wasafiri ili kuona canter za single au double cabin pekee.

Canter yenye sehemu mbili za abiria Canter yenye sehemu moja ya abiria


3. Chagua kulingana na uzito wa mizigo itakayobebwa

Canter za Mitsubishi zipo kwenye kundi la malori madogo na hata canter zenyewe zipo za aina mbili, canter za kawaida na canter guts. Tofauti kubwa baina ya hizi canter mbili ni uwezo wa kubeba mizigo ambao umegaanywa katika makundi mawili:

  • Canter za kubeba tani 2 au Zaidi
  • Canter guts zenye uwezo wa tani 1.5 au chini ya hapo

Kwa mfano, lori kubwa zaidi kati ya malori ya Mitsubishi ni haya yafuatayo:

  • Fuso fighter yenye uwezo wa kati ya tani 3.5 hadi tani 4
  • Fuso super great yenye uwezo wa kati ya tani 5 hadi tani 10 au Zaidi

Unaweza kuweka order ya canter (lori) kulingana na kiwango cha mzigo (uzito) ambao gari linaweza kubeba. Kwa Mfano, ikiwa unahitaji lori la tani 4 unaweza kutafuta katika tovuti yetu ya CardealPage kwa kuainisha uzito huo.

Hata hivyo, kuna aina nyingi za malori kwa matumizi maalumu na tofautitofauti.
Uwezo wa lori kubeba mzigo mkubwa/mdogo unategemea mambo yafuatayo;

  • Urefu wa bodi/jukwaa la lori husika (urefu wa sehemu ya mzigo)
  • Ukubwa wa matairi
  • Sehemu za abiria kukaa (mstari mmoja au miwili)
  • Uzito wa fremu ya canter

Kabla ya kununua canter (lori), tunashauri uzingatie sana  uwezo wa gari ktika kubeba mizigo (Loading capacity), ujiridhishe na mwonekano (picha) za gari husika, nk. kisha wasiliana na wauzaji.






Pia, unaweza kuangalia loading capacity (uwezo kubeba mizigo) wewe mwenyewe.
Kwa kuangalia nyuma ya gari (sehemu ya nyuma ya bodi ya gari) unaweza kuona stika zenye maandishi kama 1500 Kg, 2000 Kg, 3000 Kg, nakadhalika.

Japokuwa yawezekana usiwe na matatizo katika kutumia tovuti/ukurasa wa CardealPage, Tumeona mara kadhaa wauza magari walaghai wachache wakidangaya kwa kuweka sticker wanazochukua mitandao mingine na kubandika humu.

Ili kukwepa udanganyifu wa aina hii,  ni muhimu kutizama taarifa zinazohusiana na uwezo wa kubeba mizigo wa gari katika nyaraka/hati rasmi  za gari (Vyeti vya kutuma gari nje ya nchi n.k).

Ukiweza, ni vyema ukaomba kupata taarifa na nyaraka hizo kutoka kwa anayeuza gari husika.

Magari (malori) yote yanayowekwa katika tovuti ya CardealPage, unashauriwa kutumia huduma ya hiari ya Cardeal Inspection.

Kwa kutumia huduma hii ya Cardeal Inspection, tovuti ya CardealPage inakusaidia kuangalia usahihi wa nyaraka za gari husika kabla ya gari kutumwa kwako, na CardealPage watarejesha fedha zako iwapo taarrifa za gari ni tofauti na zilizooneshwa kwako kwahivyo hupaswi kuogopa kuhusu hilo.

Kwa hiyo, kwa mujibu wa uwezo wa gari katika kubeba mzigo au uzito flani, lori au canter za Mitsubshi zinaweza kuwekwa katika makundi yafuatayo:

  • Canter guts zenye uwezo wa tani 1.5 au pungufu
  • Canter za tani 2 hadi 3
  • Fuso fighter zenye uwezo wa kati ya tani 3.5 hadi tani 4
  • Fuso super great za tani 5 hadi tani 10 na kuendelea

Na sasa, tunaamini umekwisha fahamu aina ya canter/lori unalohitaji.

Na kwakweli, baadhi ya wauza magari wa Japan hutumia jin ala canter kumaanisha au kujumuisha aina zote tajwa hapo juu (canter guts, fuso fighter, n.k.) na hii ni kwa sababu hata wao wenyewe hawafahamu tofauti baina ya hizi aina 4 za canter tulizokwisha kuzitaja.

Ikiwa unahitaji canter guts za uwezo wa tani 1.5 au pungufu, unaweza ukajaribu kutafuta kwa kuandika neno “Canter” na ukafanikiwa pia.




4. Chagua kwa Kuzingatia Aina ya Mafuta Yanayotumiwa na Gari

Kuna aina kadhaa za mafuta zikiwemo petroli, disel na LPG.
Aina nyingi za canter na canter guts zinazouzwa Japan huwa zinatumia diesel.  Canter zenyewe zipo za diesel pekee isipokuwa kwa canter guts zipo zinazotumia diesel na baadhi hutumia petrol .

Bei za malori ya canter yaliyokwisha kutumika nchini Japan zinaongezeka kwa kufuata mpangilio ulioneshwa hapa chini, (ikiwa zimetumika kwa miaka na umbali unaolingana na zina maumbo/ukubwa, na uwezo unaofanana n.k.).

Dizeli >  Petroli > LPG

 Canter (lori) za diesel zina bei kubwa Zaidi .

Kwanini Canter (Lori) za Diesel Zinahitajika Zaidi?

 
Ukitizama tofauti baina ya magari yanayotumia diesel na petroli utagundua kwamba yanayotumia diesel ni mengi zaidi.

Sifa za Magari Yanayotumia Petroli
  • Kwa sababu petroli huzalisha nguvu (power) kidogo, huwa sio nishati sahihi kwa magari yanayobeba mizigo mizito.
  • Injini za magari ya petroli hutoa milio midogo na mara nyingi huwa na mwendo wa kasi sana kuliko zinazotumia dizeli.
  • Gharama za uzalishaji huwa ndogo kuliko zile za dizeli.
Sifa za Dizeli
  • Ni nzuri zaidi kubeba mizigo mizito na hutumika katika mashine za uzalishaji na ujenzi kwakuwa huzalisah nguvu (power) zaidi
  • Hutoa nguvu zaidi na sio kasi
  • Gharama za uzalishaji huwa kubwa kuliko za petroli

Torque ni kitu gani?

* Torque ni neno la kiingereza limaanishalo nguvu inayosababisha mzunguko na katika magari, tunatumia neno torque kuelezea nguvu inayosababisha mzunguko wa ijini. Unaweza kuelewa zaidi ikiwa utaanza kuifikiria pedeli ya baiskeli.

Wakati unapoanza kunyonga pedel ya baiskeli, mwanzo kabla baiskeli haijaanza kutembea, nguvu zaidi huhitajika kuifanya itembee, Lakini inapoanza kwenda kwa kasi unahitaji nguvu kiasi tu ili kuifanya baiskeli iendelee kutembea.

Unaweza kuifikiria katika nadharia hiyo, kwamba “torque huwa kubwa” wakati unapoanza kunyonga pedeli ya baiskeli na kuifanya baiskeli kuanza kutembea kitu ambacho hushabihiana na injini za magari pia.

Injini za Dizeli huwa na gharama kubwa pamoja na gharama za uzalishaji wa nguvu ya kusuka injini, lakini magari na haswa malori ya mizigo yatumiayo nishati hii huwa na nguvu sana ya kubeba mizigo mizito. Na kwa sababu hiyo, dizeli ndio nishati kubwa zaidi na maarufu katika magari ya mizigo kuliko petroli.

Matokeo yake ni kwamba, uhitaji wa magari ya diesel toka kwa wanunuzi waishio nchi tofauti na Japan ni mkubwa suala ambalo linaleteza gharama za magari haya kuwa juu pia.





Tahadhari Dhidi ya Injini za LPG

Hata nchini Japan, injini za LPG (liquefied petroleum gas) hazitumiki sana. Matumizi ya injini hizi ni madogo mno na yameruhusiwa kwa baadhi ya taasisi za serikali kwa matumizi maalum, na hivyo uzalishaji na matumizi ya injini hizi ni mdogo mno karibu sawa na kusema hayapo kabisa au hazihitajiki.

Kwa sababu hii, bei za magari yanayotumia injini hizi huwa chini sana na baadhi ya wanunuzi hushawishika kununua sababu ya urahisi pasipo kuelewa na huishia kufanya maamuzi na manunuzi yasiyo sahihi.

Utawasikia wakisema, “Loooh, gari hii inauzwa bei rahisi kweli, wacha ninunue kabla hawajalichukua wengine!!”
Hata ikiwa utawaza hivyo,  Ni vyema ukapitia tena taarifa za gari husika ukiwa umetuliza akili yako kujiridhisha kwamba haitumii injini ya LPG.  Hata hivyo, katika nchi ambazo magari yanayotumia injini za LPG yanaruhusiwa, wanaweza kununua kwa bei rahisi na hivyo kuokoa fedha zao nyingi.

Kufikia hapa, kwa kiasi kikubwa nimezungumzia namna ya kuchagua canter.

Suala la nguvu (power) inayohitajika ni la msingi sana na kwa mantiki hiyo injini za diesel tunashauri ndio iwe chaguo lako la kwanza katika kununua gari za mizigo mizito.
Nunua gari inayotumia injini ya petrol kwa ajili ya kubebea mizigo myepesi tu na kusafiri kwa mwendo wa haraka.

Katika Makala inayofuata, tutazungumzia namna ya kutathmini injini ya gari.

IFUATAYO>> Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Kununua Lori za Mitsubishi (Mitsubish Canter) Sehemu ya 02




-Taarifa muhimu, Uelewa

Copyright© CardealPage , 2024 All Rights Reserved.