Taarifa muhimu Uelewa

Vidokezo 10 Muhimu vya Kuzingatia Wakati wa Kununua Lori za Mitsubishi (Mitsubish Canter). Sehemu ya 02

Last updated:


Mara ya mwisho, nilielezea Vidokezo muhimu vinne katika kuchagua na kununua canter.

Makala iliyopita >> Vidokezo 10 Muhimu Vya Kuzingatia Katika Kununua Lori za Mitsubishi (Mitsubishi Canter) Sehemu ya 01

  1. Chagua Muundo wa bodi (sehemu ya mzigo)
  2. Chagua idadi ya abiria wanaoweza kupakiaa katika canter
  3. Chagua uwezo wa gari katika kubeba mizigo (loading capacity)
  4. Chagua aina ya mafuta yatakayotumika katika gari

Sasa, tutaelezea vidokezo vingine 6 vya muhimu ikiwa ni pamoja na masuala ya injini.

5. Chagua aina ya injini

Tutazungumzia aina za injini ambazo mnunuzi anaweza kuwa na maswali kuzihusu.

Injini za canter za Mitsubishi huwa ni za Dizeli kama vile 4D33, 4M40 na 4M50.
 Injini za 4D ni maarufu sana na hupendwa Zaidi na wanunuzi toka nchi tofauti na Japan. 

Injini ya 4D30 Injini ya 4D32 Injini ya 4D33
Injini ya 4D34 Injini ya 4D35 Injini ya 4D36
Injini ya 4M40 Injini ya 4M50 Injini ya 4M51
Injini ya 4P10
(Baada ya Novemba. 2010)
 Malori aina ya canter guts hayana modeli ya 4D, aina pekee ya inayopatikana katika canter guts ni 4M. 

 Japokuwa canter zinazo aina hizi za injini (4M & 4D), Injini aina 4M huwa na bei rahisi ikilinganishwa na 4D. Hivyo basi, ni muhimu kuzingatia matumizi pamoja na bei/gharama ya Injini husika. 

3. Hebu tufahamu zaidi kuhusu injini maarufu za 4D

Canter zenye injini za 4D huuzwa pia katika tovuti ya CardealPage.
Tuziangalie kwa ukaribu aina hizi za injini.

“4” katika Injini za 4D zinamaanisha silinda 4. Na D inasimama kwa ajili ya Diesel na strokes 4 hutumika katika Injini za 4D.

Stroki 4 (4 strokes) humaanisha kuwa mchakato wa kuunguza nishati, Mfano, kuingiza hewa, mgandamizo wa hewa, uchomaji wa gesi (fuel), unafanyika jkatika hatua 4.

Mwaka 1978, canter za 4D30 ndio zilizinduliwa na kutumika kwa mara ya kwanza, na baada ya hapo zimeboreshwa sana na kuwa na matoleo mapya ya 4D31 pamoja na 4D32.


Uhamishaji (kiwango cha nishati) cha Injini hizi ni kama ilivyobaishwa hapa chini.

Aina ya InjiniUkubwa/Kipimo wa Injini 
4D303.3L
4D313.3L(Inakuwa na injeksheni ya Dizeli ya moja kwa moja)
4D323.6L
4D334.2L
4D343.9L
4D354.5L
4D363.6L

Injini maarufu Zaidi katika tovuti yetu ya CardealPage ni za Lita  4.2 L 4D33.  Zinakuwa na uhamishaji (displacement) na nguvu kubwa nah ii inazifanya kuwa maarufu zaidi.

Kama ilivyoelezwa kabla,  canter hazina mpangilio wa petroli (hazitumii petroli). 
Injini zinazotumia petroli ni za canter ndogo (canter guts) zinazotumia 4G63.

6. Chagua kwa Kuangalia Urefu wa Mgongo wa Sehemu ya Mzigo

Tumezungumzia vidokezo vingi ambavyo kwa ujumla wake vinaweza kupatikana katika nyaraka rasmi za gari husika.

Sasa hebu tuone mazingira ambayo uchaguzi na maamuzi yanaweza kuwa magumu ikiwa hujui gari husika. Nakushauri kutizama picha hizi zifuatazo.

Kuna aina 3 tofauti za urefu wa sehemu za mizigo za canter. Zimegawanyika katika  “Mgongo Mrefu, “Mgongo Mnyoofu Mfupi”, na “Mgongo Mfupi”. 

Mgongo Mrefu Mgongo Mnyoofu Mfupi Mgongo MfupiNchini Japan, canter za mgongo Mnyoofu Mfupi na mgongo Mfupi zipo nyingi tu, lakini hakuna jina moja linalotumika kuzitambulisha canter zenye mgongo Mrefu.
 Hata hivyo, wanunuzi wengi magari yenye mgongo mrefu huziita lori zenye sehemu ya mzigo iliyoinuka (ya juu) na matumizi haya ya maelezo yanatumika mara nyingi Zaidi na wauzaji huyaelewa. 

Hali za pahala pakupakia mizigo kwa aina hizi tatu za canter zimeelezwa hapa chini.

Mgongo Mrefu
*”Mgongo Mrefu” sio neno maarufu san kwa wauza magari wa Japan, Lakini wanunuzi toka nchi tofauti na Japan hulitumia Zaidi na ni neno maarfufu kwa wanunuzi

 • Kichwa cha gari kinakuwa kinalingana na urefu wa mgongo wa sehemu ya mzigo
 • Magurudumu ya mbele na nyuma yanalingana an huwa na saizi ya nchi 16 au zaidi
Mgongo Mnyoofu na Mfupi
 • Magurudumu ya mbele na nyuma yanalingana
 • Sehemu ya kubebea mzigo huwa chini kidogo ya ikilinganishwa na kichwa
Mgongo Mfupi
 • Magurudumu ya mbele na nyuma yanakuwa na ukubwa tofauti, Gurudumu za nyuma huwa ndogo kuliko za mbele
 • Sehemu ya kubebea mzigo huwa chini zaidi ikilinganishwa na kichwa
 • Magurudumu ya nyuma yanaweza kuwa mawili

Zaidi ya hayo, canter zenye mgongo Mfupi hazitambuluki (sio maarufu sana) nje ya Japan, lakini kutegemeana na mnunuzi nan chi anayotoka canter hizi hujumuishwa katika kundi la canter zenye mgongo Mrefu na huandaliwa magurudumu ya nchi 16.
Tofauti katika utambuzi wa aina hizi za canter umeonekana katika nchi tofautitofauti kwa majina mbalimbali.

Ni kwanini Nchini Japan kuna canter za Mgongo Mfupi?
Nchini Japan, barabara huwa za lami tambarare miji yote na kwa sababu hiyo hakuna makorongo na mashimo katika barabara isipokuwa katika maeneo ya ujenzi yaliyopo milimani.

Wakati wa kupakua na kupakia mizigo, kazi ambazo hufanywa na gari hizi huwa ni chache na ndogo na mara nyingi gari hizi huwa sokoni baada ya muda mfupi.

Kwa upande mwingine, nchi tofauti na Japan, barabara huwa sio rafiki sana na huwa na makorongo mengi kwa kwa sababu hii canter za juu na zenye mgongo Mrefu hupendelewa Zaidi.


Elewa Tofauti ya Vifaa Vilivyopo Sehemu za Chini ya Gari

Gari za abiria huwa na springi maalum za kuzuia au kupunguza mshtuko/mtikisiko ili kumfanya Msafiri aweze kuwa katika hali ya utulivu na kuifurahia safari yake awapo safarini.

Hata hivyo, Ikiwa utabeba mizigo mizito springi hizi maalumu huharibika.

 Kwa upande mwingine, magari ya biashara kama canter hutumika kubeba mizigo mizito na hii ndiyo sababu springi maalum (Tizama picha hapo chini) zimekuwa maarufu na hutumika Zaidi. 

Vifaa maalum vya kupunguza mtikisiko na mshtuko kwa kutumia vijisahani maalum vya chuma ni maaufu zaiidi.

Vifaa hivi ni imara sana na uvunjikaji wake ni mgumu mno na hivyo vimekekuwa maarufu na hutumika Zaidi katika magari ya mizigo.

Badili Bei Wakati wa Kuweka Springi

 Bei za canter na matumizi huathiriwa na mahali springi zinapofungwa katika gari husika. 

Kuna sehemu mbili ambapo springi zinaweza kufungwa kama inavyoonekana hapa chini.

 “Juu ya Gango”  Springi zinafungwa juu ya shafti (juu ya differential gear)  “Juu ya Gango”  Springi zinafungwa chini ya shafti (chini ya differential gear)

Endapo springi zitafungwa chini ya differential gear, zinaweza kuharibiwa na ubovu wa barabara (makorongo, mawe n.k.) kama ambavyo ilikwisha elezwa awali.
Kwa sababu hiyo, springi hufungwa juu ya shafti (juu ya differential gear) katika magari yaliyo mengi. 

Zaidi ya hayo, upo uwezekano wa kuzikuta springi zikiwa zimefungwa chini ya shafti (differential gear)  hata katika magari ya juu ya mgongo Mrefu, ni muhimu uwe makini. 

Gari za juu za mgongo Mrefu, huuliziwa na kununuliwa zaidi na wanunuzi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia na hii ni kwa sababu haziathiriwi sana na ubovu wa barabara.

Hata hivyo, gari hizi sio nyingi sana nchini Japan na hivyo bei huwa juu sana na upatikananji wake ni mgumu kiasi.

Kuhusu Matairi

Matairi mawili ya nyuma mara nyingi hufungwa katika gari za biashara za kubeba mizigo, lakini wakati mwengine gari hizi huwa na tairi moja nyuma.
Na kwa mantiki hiyo, kwa kuongeza ukubwa wa gurudumu (tairi) za nyuma kunawezesha canter kuhimili uzito mkubwa na hivyo canter za mgongo Mrefu za juu za tairi moja nyuma huuliziwa sana na wateja pia kama za magurudumu mawili.

Kwakuwa canter za mgongo mrefu za tairi moja nyuma hutumika kubeba magazeti nchini Japan,  hali za canter hizi zinakuwa zikiuzwa huwa nzuri sana ikilinganisha na zile zinazotumika katika ujenzi au migodini.  Uhitaji huwa ni mkubwa lakini upatikanaji ni mgumu.7. Chagua Gari Manual Au Automatic

Malori (canter) mengi ya nchini Japan huwa ni manual.
Hata hivyo, kwa ajili ya urahisi wa matumizi, canter amabzo ni auto zinaweza kupatikana mara chache.

 Endapo utapata lori la bei nafuu, inaweza kuwa auto na hivyo ni muhimu kuangalia hili kwa umakini. 
Gia ya Manual Gia ya Auto

    

8. Chagua canter ya 2WD au 4WD

Kimsingi, 2WD inatumika zaidi kwa gari ndogo za mizigo nchini Japan. Hata hivyo, wanunuzi toka nchi zingine nje ya Japan hupendelea zaidi 4WD na hii hufanya gari hizi kuwa na bei kubwa.

Matokeo yake, upatikanaji wa canter za 4WD ni mgumu kiasi na kwa sababu hiyo ni vyema kufikiri upya ikiwa mahitaji yako yanastahili ununue gari ya 4WD.

Ikiwa utaamua kununua 4WD, hebu sasa tuelewe tofauti iliyopo baina ya aina hizi mbili, 4WD na 2WD ili usije ukanunua 2WD kimakosa.

Itambue 4WD kwa Kuangalia Sehemu za Chini ya Gari

Unaweza kutofautisha 4WD na 2WD kwa idadi ya differential gears.

Alama nyekundu katika picha hizi mbili zinaonesha gia ya kubadilishia (differential gear).
 Ikiwa kuna gia mbili za kubadilishia (differential gears) mbele na nyuma gari hiyo ni 4WD na ikiwa kuna gia moja tu yakubadilishia (differential gear) nyuma ya gari basi hiyo ni 2WD. 

Wakati wa kuangalia picha za chini ya gari,sio rahisi kuigundua tofauti hii.
Ikitokea hivyo,ni vyema kuangalia endapo ina tairi moja au matairi mawilimawili ya nyuma.

Kimsingi,  lori huwa na tairi moja mbele na tairi mbilimbili nyuma (tairi moja nyuma huwepo mara chache sana). Kwahivyo unaweza kuichukulia picha kwamba ni sehemu ya nyuma ya gari.

Namna nyingine ya kugundua ikiwa gari ni 4WD au 2WD ni kuangalia endapo gari ina sehemu ya katikati ya differential gear.

Sio muhimu sana, Lakini fahamu pia ya kwamba nembo ya 4WD inaweza kubandikwa hata katika gari ya 2WD.
Niliopokwenda Thailand kwa safari ya kibiashara, nilishangaa sana nilipoona gari za 2WD zikiwa zimebandikwa stika zenye nembo ya 4WD. Hili lilionekana kuwa jambo la kawaida sana nchini Thailand.

Kuangalia ikiwa Gari ni 4WD kwa Kutizama Switch ya Kubadilishia

Magari madogo hutumia 4WD mara chache na sio muda wote huwa 4WD.

4WD za muda mfupi zinakuwa na swichi ya kubadilishia ya 4WD jirani na kiti cha dereva kama inavyooneshwa katika picha hapa chini.  Kwahivyo endapo utaona picha hii unaweza kutambua yakuwa gari husika ni ya 4WD. Namna ya Kutambua 4WD kwa Kutumia Modeli

Kwa mara nyingine tena, unaweza kutambua ikiwa gari ni 4WD kwa kutumia code za modeli.
Ikiwa D ipo na inasoomeka katika code za model ya canter kama vile FD*, basi gari hiyo ni 4WD.
 Ikiwa picha ulizotumiwa na muuzaji hazionekani vizuri, basi waweza kuitambua 4WD kwa namna hiyo. 

Tizama hadithi hii kuhusu uendeshaji wa malori.
Malori yanayouzwa Japan mara nyingi huwa ni 2WD FR (kumaaniasha front engine/rear drive) na ni rahisi kusema uendeshaji kwa kutumia tairi za nyuma ni maarufu zaidi.

Ni kwanini basi kuna magari mengi sana ya FR? Hi ni kwa sababu, baada ya kupakiza mizigo katika bodi la mzigo, upande wa nyuma wa lori unakuwa umebeba mzigo mkubwa sana na hivyo nguvu Zaidi huhitajika ili kuubeba.

Ikiwa FF (front engine/front drive) zinatumika kubebebea mizigo mizito, matairi ya nyuma yanakuwa hayajalemewa na hivyo huweza kuinuka juu na kushinda kusukuma gari liende mbele.
Hii ndiyo sababu magari mengi ya mizigo yanakuwa ni FR kitu ambacho husababisha nguvu ya kuendesha gari kuwa imelemewa na mzigo sehemu ya nyuma ya gari.


9. Chagua kwa Kuzingatia Hali ya Gari

Pointi ya mwisho ni kuzingatia hali ya gari wakati wa manunuzi.
Malori yanasemekana kuwa na hali mbaya kuliko gari za abiria kutokana na matumizi yake.
Ni muhimu sana kuwa makini na  kutu na kulika/kubanduka kwa gari .

Ni aina ipi ya kutu ya kuwa makini nayo sana?  Bado inakubalika ikiwa kutu inaokena bado kuwa na rangi nyekundu kwa juu juu.  Lakini kwa upande mwingine, kuwa makini sana na matobo yatokanayo na kutu iliyokula chuma kwa muda Mrefu.

Ikiwa kutu imekula sana, hata bei nayo lazima iwe ya chini. Kwahivyo, nunua kwa bei ya chini kisha kaifanyie matengenezo baada ya kuwa gari imekufikia. Hii ni nzuri ukiifuata.

Ikiwa huwezi kukadiria gharama za matengenezo kabla ya kununua,  kuwa makini usinunue kwa bei ya juu sana gari chakavu. 

Endapo utanunua gari likiwa katika hali mbaya kwa bei nafuu, ushuru wa forodha huwa nafuu. Kwahivyo, manununuzi yako yanaweza kuwa na faida. Ikiwa wewe mwenyewe ni fundi magari au unae fundi mzuri, waweza fanya biashara nzuri sana kwa namna hii.

10. Dondoo Pekee Kuhusu Gari za Breki za Upepo (4T)


Hiki ni kifaa ambacho kinapatikana katika gari za  breki za upepo (tani 4 na zaidi).
Breki za upepo zinauwezo mkubwa sana wa kuzuia au kusimamisha gari kuliko breki za majimaji (hydraulic).
Hivyobasi, tofauti na malori makubwa hata canter za tani 4 zinafungwa breki za upepo wakati mwingine.

Ikiwa unapanga kununua lori la tani 4 au Zaidi ni vyema ukatizama na kuzielewa breki za upepo.
Ikiwa unaona gari yako ikipakia mizigo mizito sana, tunashauri ununue canter za saizi ya kati ambazo zinatumia breki za upepo.

Chakujua tu ni kwamba, bei itakuwa juu kiasi. Ikiwa unasadiki kuwa mizigo haitakuwa mizito sana, basi hauhitaji kuwa na gari za kutumia breki za upepo na hivyo utatumia fedha kiasi kununua zenye breki za kawaida.
Hata hivyo, wacha tuone ikiwa ni sahihi kwa matumizi uliyokusudia.

Canter za Mitsubishi zenye kutumia breki za upepo ni Fuso Fighter na Fuso Super great.


Nimeshazungumza namna ya kuchagua canter mpaka kufika hapa.
Ikiwa unahitaji kununua canter yenye matumizi yanayoendana na uhitaji wako, bei haitakuwia tatizo sana.
Chagua canter kulingana na matumizi yako an hakikisha mahitaji yako ya chini kabisa yanafikiwa nah ii itakusaidia kupata gari sahihi.

 Tafadhali, Fikiria ni aina gani ya canter unaihitaji na kisha fanya manunuzi. 

Ndani ya tovuti ya CardealPage, wauzaji wengi wa magari ni makampuni makubwa.
Ukihitaji kununua canter za Mitsubishi, tafadhali usiache kutizama stoo ya CardealPage

-Taarifa muhimu, Uelewa

Copyright© CardealPage , 2024 All Rights Reserved.