Inawezekana umepanga kununua basi dogo toka Japan kama vile COASTER, ROSA, au CIVILIAN.
Wakati wa kununua, ikiwa utakuwa unaelewa aina hizi za mabasi madogo na jinsi ambavyo hutumika Japan, unaweza kukadiria kwa usahihi hali ya basi husika wakati unalinunua.
Katika ukurasa huu, tutakupa vidokezo na dondoo chache za kukusaidia katika kufanya maaui sahihi.
Elewa Watengenezaji wa Mabasi Madogo, Modeli Zake na Miundo
Modeli kuu na maarufu zaidi za mabasi madogo ni hizi zifuatazo:
TOYOTA COASTER
MITSUBISHI ROSA (MITSUBISHI FURO)
NISSAN CIVILIAN
HINO LIESSE (LIESSE2)
ISUZU JOURNEY
Kimsingi hizi ndizo aina kuu za mabasi madogo yanayouzwa na kutumwa nje ya Japan.
Angalia Usahihi wa OEM na Ufanye Maamuzi ya Busara
Mara nyingi canter hutofautiana maumbo kulingana na mwaka yalipotengenezwa na modeli.
Hata hivyo, japokuwa watengenezaji na majina huwa tofauti, mara nyingi huwa na mwonekano unaofanana ikiwa ni matokeo ya OEM.
Kwa Mfano, ukitizama picha za TOYOTA COASTER, HINO LIESSE, NISSAN CIVILIAN pamoja na ISUZU JOURNEY, zinakaribia kufanana.
-COASTER Modeli yake ni HZB50
-LIESSE Modeli yake ni HZB50M
Tofauti pekee baina ya modeli za Liesse na Coaster ni herufi “M” iliyoongezeka katika modeli namba ya Liesse.
Hii inalandana hata katika modeli za Civiliana pamoja na Journey.
CIVILLIAN Modeli yake ni BVW41
JOURNEY Modeli yake ni SBVW41
Modeli namba ya JOURNEY huanza na herufi S.
Japokuwa majina ya modeli za OEM hutofautiana, staili zake na miundo hukaribia kufanana.
Kwa sababu hiyo, tekniki makini katika ununuzi wa gari hizi ni kutafuta gharama za gari zenye modeli sawia na kufanya ulinganifu wa gharama ili kupata gari ya bei nafuu.
3. Sababu za Mabasi Madogo Yanayouzwa Japan Kuwa Katika Hali nzuri
Mabasi madogo ya Japan unapoyalinganisha nay ale ya nchi zingine utagundua yanakuwa katika hali nzuri wakati yakiuzwa ukilinganisha nay ale ya nchi zingine.
Sababu ni hii:
2. Mabasi madogo hayatumiki kwa safari ndefu na hivyo wakati wa kuyauza yanakuwa hayajatembea umbali Mrefu sana
3. Yanakuwa yanaendeshwa na madereva wenye sifa stahiki
Kila mwaka mabasi madogo hukaguliwa ndipo yanapewa kibali cha kuendelea kutumika
Magari yanapotumika kibiashara nchini Japan, ni lazima yafanyiwe ukaguzi kila mwaka kwa mujibu wa sharia za Japan.
Ili gari liweze kufaulu na kupitishwa katika ukaguzi huu, sehemu mbovu za gari lazima ziondolewe na kufanyiwa service kubwa na kwa sababu hii, hali za mabasi madogo yanayotumika Japan kamwe hayawezi kuwa mabovu kiasi cha kuogofya na mar azote yanakuwa vizuri.
Hayatumiki kwa masafa marefu na hivyo yanakuwa yametembea umbali mdogo wakati yanapouzwa
Sifa nyingine ya mabasi madogo ya Japan ni hii, kwamba hayaendi mwendo Mrefu. Na kwa sababu hiyo, huwa yanakuwa katika hali nzuri.
Matumizi ya mabasi madogo nchini Japan ni kama Yafuatavyo:
- Kubeba watoto kwenda shule/nyumbani
- Kusafirisha wanafunzi wa mashule ya kuogelea
- Kusafirisha misiba na maharusi
- Kusafirisha watalii kwenda maeneo yenye vivutio
- Kusafirisha wana habari
- Kusafirisha walemavu
- Kukodishwa
- Na mambo ya camping
Ukiondoa biashara ya kukodisha mabasi Japan, kama unavyoona katika orodha hiyo hapo juu matumizi ya basi ndogo Japan ni ya mwendo mfupi toka sehemu A kwenda sehemu B.
Mabasi makubwa hutumiwa kwa masafa marefu nchini Japan na kwa sababu hiyo mabasi madogo yanpona shuruba hii na kua na umbali mfupi.
Mabasi madogo huendeshwa na madereva wenye sifa
Ili kupewa leseni ya kuendesha mabasi madogo nchini Japan, madereva lazima wawe na leseni za sifa stahiki ambazo huwa ni tofauti na leseni za kuendeshea magari ya kawaida.
Kwa sababu madereva wa mabasi haya ni wazoefu na wameelimika, hali za magari haya zinaendelea kuwa nzuri wakati wote sababu hawayaendeshi kwa fujo kama ambavyo watu wasio na sifa na uzoefu wangefanya.
Kwa sababu hizi tatu za msingi, hali za mabasi madogo toka japan huwa ni nzuri ukilinganisha na za nchi zingine.
Hata hivyo, kuna mazingira ambapo kutu zitokanazo na mazingira ambapo mabasi haya huhifadhiwa kama vile pembezoni mwa bahari au milimani husababisha gari hizi kuharibika kiasi. Kwa hivyo unapaswa pia kuwa makini na kufanya ukaguzi wa nje kaba ya kununua.
Namna ya kutathmini jinsi ambayo basi dogo limekuwa likitumika
Ipo namna ambayo unaweza kugundua basi husika lilitumika kufanya shughuli za aina gani huko Japan. Tutakupatia siri katika kipengele hiki.
Ili kuweza kufahamu matumizi ya basi husika huko Japan, unalazimika kuangalia Logo na lugha iliyotumika katika basi husika.
Kwa Mfano, kama tulivyoonesha katika picha hapo juu ikiwa kuna alama ya pembe tatu ya rangi ya njano katika bodi ya gari husika, basi tambua kwamba basi hilo lilikuwa likitumiwa kusafirisha watoto wa shule za awali.
Hili lipo hivyo hata kwa mabasi mengine. Kijapani kilichocandikwa katika bodi za magari haya zinakupatia picha ya matumiz ya basi husika huko litokako.
Kwa Mfano:
- xxxxxx school (kumaanisha shule)
- xxxxxx school (shule ya kuogelea)
- Jina la kampuni (ukitafuta kampuni husika mtandaoni utajua matumizi ya gari hilo katika kampuni husika)
- Jina la mahali. (kutegemeana na eneo, unaweza pata wazo (idea) endapo gari husika limeliwa na kutu na mambo mengine)
Kwa njia hii, ikiwa unaelewa kijapan unaweza kukisia namna ambavyo basi limekuwa likitumiwa na mmilikiwa wake kabla ya kuuzwa na hii itakusaidia kufanya manunuzia salama.
Wakati mwingine, Jaribu kumuuliza mtumishi yeyote wa tovuti ya Cardealpage akupe maelekzo na maana ya maneno yaliyoandikwa katika bodi ya gari unayotaka kuinunua.
Tovuti ya CardealPage huwa na orodha ya mabasi madogo yasiyopungua 150 na hii inakufanya uwe na uwanja mpana wa uchaguzi na kuifanya pia tovuti hii kuwa kinara wa kuuza mabasi ya aina hii.
Kwa yeyote anaetazamia kununua basi dogo, tunashauri kutembelea ukuras awa Cardealpage.