Katika kurasa na tovuti yetu ya CardealPage mara nyingi tuposti na kuuza basi ndogo za MITSUBISHI ROSA.
Basi hili moja la Rosa lina matumizi tofauti na bajeti za wanunuzi pia hutofautiana kulingana na uwezo wao na namna ambavyo Rosa inaweza kukidhi mahitaji yao, na kwa kuyazingatia haya tutakujuza namna ambavyo unaweza luchagua Rosa kulingana na mahitaji yako.
Rosa ni Maarufu Zaidi Kama Basi Ndogo za Watoto
Nchini Japan, Kuna namna tatu za jinsi ambavyo Rosa hutumika:
- Hutumika kama mabasi ya safari za watoto wa shule
- Mabasi ya watoto wadogo wa shule za awali
- Matumizi mengine ya Rosa ni pamoja na kwendea kempu na matumizi mengine maalum kama huduma za mazishi na huduma zingine binafsi
Basi Ndogo za Kutolea Huduma za Usafiri
Basi Ndogo za Watoto wa Shule za Awali
Basi Maalum Kwa Ajili ya Kambi (Camping)
Basi Maalum Kwa Ajili ya Kusafirisha Miili na Wafiwa
Zifuatazo idadi (asilimia) za mabasi madogo ya Rosa yanayouzwa katika Tovuti ya CardealPage.
Mabasi madogo ya biashara (kwa watu wazima): 40%
Mabasi ya huduma maalum (mazishi n.k.): chini ya 1%
Kama uonavyo, wateja wetu wengi hununua Rosa zilizokusudiwa kwa ajili ya wanafunzi (watoto was shule za awali).
Tofauti baina ya Rosa kwa ajili ya watoto wa shule na Roa za watu wazima (za biashara ya kusafirisha abiria) ni hizi zifuatazo:
- Muundo na mpangilio wa viti
- Urefu wa pahali pa kusimamia. (Rosa kwa ajili ya watoto huwa na sakafu za juu na kufanya kukaribiana na paa lakini ia vioo na viti vinaweza kubalishwa namna vilivyopangwa)
Sababu ya Rosa za watoto kuwa maarufu zaidi ni kwa sababu zenyewe zinaweza kubadilishika kirahisi na kwa gharama nafuu kutoka kuwa za watoto na kufanyia biasha ya usafirishaji tofauti na ilivyo kwa Rosa za abiria (watu wazima)
Rosa.
Rosa za watoto wa shule gharama zake ni ndogo karibu sawa na nusu ya gharama ya rosa za abiria watu wazima.
Hata katika soko la ndani la Japan, bei ya Rosa za watoto ipo chini kuliko za abiria.
Sio tu kwamba gharama ni rahisi katika manunuzi bali pia ushuru wa kuagiza magari haya maalumu ya watoto wa shule upo chini.
Kwa Mfano, hata kama Rosa mbili zina modeli sawa, matumizi yaliyokusudiwa ikiwa ni ya watoto wa shule au abiria yanaweza kusababisha tofauti inayoweza kufikikia dola $3,000 kati ya mabasi haya mawili yanayofanan modeli na kutofautiana matumizi.
Japokuwa mnunuzi atalazimika kulipa ushuru wa kusafirishia gari, lazima uweke akilini kwamba nchi zilizo nyingi duniani, nje ya ushuru wa forodha mnunuzi analazimika kulipa na kodi zingine pia kwa mujibu wa nchi husika.
Katika hali ya namna hii, tuseme bei ya CIF kwa Rosa ya watu wazima ni dola elfu 10 ($10,000) wakati ambapo CIF ya Rosa ya watoto ni $7,000.
Ukijumlisha na ushuru wa kusafirishia, kila gari litakuwa limelipiwa kiasi cha $18,000 na $12,600 kila moja. Hapa kuna tofauti ya $5,400.
Ukitizama tofauti ya mwanzo ya magari haya mawili ambayo ni $3,000, ushuru umeongeza gharama nyingine ya $2,400 ambayo imeongezeka kwenye Rosa ya abiria.
Kwa njia/mbinu hii unaweza kupata basi ndogo za ROSA, hivyo, tafadhali zingatia kuwa ni muhimu kununua basi dogo baada ya kuwa umewasiliana na mafundi wa magari wa eneo unaloishi.
2.Chagua Rosa yenye bodi fupi au ndefu
Bodi za Mitsubishi Rosa huwa za aina mbili, ndefu na fupi.
Kimsingi, bodi ndefu inaruhusu abiria wengi zaidi kupakia tofauti na fupi.ufuatao ni mpangilio na idadi ya abiria wanaoweza kupakia.
Huu ndio mpangilio wa msingi kulingana na nafasi/uwezo aina hizi za magari:
Bus la Saizi ya Kati (Watu Wazima) | Bus la Saizi ya Kati (Watoto) | Basi Kubwa | |
---|---|---|---|
Fupi | Ndefu | Fupi | Ndefu |
Watu 26 | Watu 29 | Watu 42 - 44 | Watu 49+ |
*Kuna wakati idadi ya abiria kwa rosa ndefu na fupi huwezi kuzijua kwa uhakika. Kwahivyo tunashauri uangalie aina na muundo wa gari.
Idadi ya Abiria kwa Basi Ndogo Zenye Bodi Ndefu
Basi ndogo za abiria zenye bodi ndefu zinaweza kubeba abiria hadi 29 kama inavyoonekana katika picha hapa chini.
Kuondoa shaka,
・Idadi hii inahusisha viti vya akiba
・Tofauti na kiti cha dereva, hakuna viti vya ziada pembeni ya dereva
Nafasi/uwezo wa kubeba abiria kwa mabasi mafupi ya abiria
Kwa upande mwingine, mabasi yenye bodi fupi ya ROSA yanakuwa yamepunguzwa mstari mmoja wa viti (viti vinne (4)) ikilinganishwa na basi zenye bodi ndefu za ROSA
Ni rahisi zaidi kwa watu kuambatanisha kiti kilichokusudiwa kuwa cha usaidizi kuwa sehemu ya viti vya abiria, na kwa sababu hii tunakuwa na jumla ya viti 26 (29 toa 4, kisha ongeza siti moja ya abiria).
Ukiziangalia ROSA, kuna wakati zinakuwa na muundo unaofanya mlango wake wa kati kuonekana kanakwamba umewekwa katika namna ya kipekee, au ikiwa friji au televisheni imepachikwa. Kwa sababu hii kuwa makini na modeli zenye muundo huu.
Idadi ya Abiria kwa Basi Ndogo Zenye Bodi Fupi
Kwa mujibu wa sharia ya Japan, Kiti kwa ajili ya mtu mzima mmoja wa Japan kinaweza kutosha mpaka mtoto mmoja na nusu kwa wenye umri chini ya miaka 12. Hii inamaanisha kwamba kwa siti moja yenye uwezo wa kukaliwa na watu wazima wawili inaweza kutumiwa na watoto watatu.
Kwa kutizama Mfano wa cheti hiki hapa chini:
-Kuna siti 3 za watu wazima, dereva, muongozaji na Mwalimu
-Viti 51 vya watoto
Katika hali hii, Tovuti ya CardealPage itahesabu idadi ya viti kuwa 54 jumla.
Kutegemeana na spicifications za gari husika, ukitizama Mfano huu wa gari ya abiria 49, tunaweza kuelewa tofauti baina ya Rosa zenye bodi fupi na zenye bodi ndefu katika idadi ya abiria.
kuwa makini, na inashauriwa kwamba utizame urefu pamoja na model number (namba ya modeli).
3.Nishati (Mafuta) yanayotumiwa na Rosa
Kimsingi, rosa zinazouzwa nchini Japan hutumia Dizeli na sio petroli.
Hatahivyo, wakati mwingine unaweza kuta baadhi ya modeli za Rosa zinatumia LPG na kwa kuzingatia hilo unapaswa kuwa makini unapofanya manunuzi.
4.Injini za Rosa
Basi ndogo za Rosa zinakuwa na Injini za Dizeli. Injini hizi zimewekwa katika makundi ya 4D** au 4M**.
Sasa, tufanye ulinganifu wa kiwango cha uhamishaji (displacement) ya hizi Injini.
4D31 | 3,290 cc |
4D32 | 3,560 cc |
4D33 | 4,210 cc |
4D34 | 3,900 cc |
4D35 | 4,560 cc |
4D36 | 3,560 cc |
4M50 | 4,890 cc |
4M51 | 5,240 cc |
Hizi ndizo Injini kuu tano za Rosa.
Nafasi | Aina ya Injini | Kiwango cha Mauzo |
---|---|---|
1 | 4D33 | 43.2% |
2 | 4D34 | 12.2% |
3 | 4M51 | 11.5% |
4 | 4D36 | 10.8% |
5 | 4D32 | 8.6% |
Kama inavyoonekana hapo juu, Injini maarufu zaidi ni 4D33.
Injini ya 4D33 ni maarufu Zaidi barani Africa.
5. Aina za Suspension za Rosa
Suspension ya nyuma ya Rosa imegawanyika katika:
・Suspensheni za springi (Leaf spring suspension)
Kuna aina mbili kwa ujumla. Lakini inayopendwa Zaidi ni ya springi.
Faida za suspensheniza za upepo ni hizi zifuatazo:
・Ni nyepesi kuvunjika ikiwa kutakuwa hakuna upepo
・Spea zake huwa ni bei ghali
Faida za suspension za springi:
Kwa upande mwingine, hasara za springi ni hizi:
・Kwakuwa springi hupata mshtuko moja kwa moja, huwa safari inakuwa na kurushwarushwa sana
Katika nchi ambazo barabara sio nzuri, tunashauri kutumia suspension za springi kwa kuwa ni nafuu na rahisi kupatikana.
Ni vipi utagundua air suspension katika matairi ya basi za Rosa?
・Ikiwa idadi ya abiria ipo chini ya kiwango cha kawaida.
*unapotafuta gari za Rosa kwa kuzingatia idai wa abiria, unashauriwa uwasiliane na wauzaji kwakuwa gari inaweza kuwa na modeli spesho.
6.Tahadhari Kuhusu Gari Ambazo ni Auto
Zaidi ya nusu ya gari za Rosa zinazopatikana Japan zinakuwa Manual. Lakini, kuna wakati za Auto zinapatikana pia.
Rosa ambazo ni Auto huwa ni bei rahisi Zaidi, kuwa makini usije nunua hizi kimakosa.
7.Rosa za 4WD ni Adimu Sana
Rosa zinazouzwa Japan maranyingi huwa ni 2WD. Hata hivyo, kuna wanunuzi wanakuwa wanatafuta Rosa za 4WD kwa ajili ya barabara mbovu za maeneo wanapotoka.
Upatikanaji wake huwa ni nadra sana kwa hiyo ukifanikiwa kupata ya 4WD na ikakidhi vigezo vyako, inunue haraka iwezekanavyo.
Ukiyazingatia haya, bei za Rosa zinaweza kutofautiana sana ukilinganisha na vigezo kama idadi ya abiria na vingine.
Tafuta Rosa ukizingatia vigezo ambavyo ni vya lazima kwako.